Full-Width Version (true/false)


MOSHI: Anaswa na umeme na kufariki wakati akifanya kibarua cha kupangua matawi ya mti

 

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Rafael Sui, mkazi wa Kata ya Shirimakunda katika Manispaa ya Moshi amefariki dunia papo hapo baada ya kunaswa na umeme wakati akifanya kibarua cha kupangua matawi ya mti uliopitiwa na nyaya za umeme.


Tukio hilo limetokea Jana may 27,2018 majira ya saa tisa za alasiri jirani na Hospital ya St.Joseph iliyopo Soweto mjini Moshi ambapo marehemu aliitwa na Neema Mbise mkazi wa eneo hilo na kumpa kibarua cha kupangua matawi ya mti mkubwa uliokuwa jirani na nyumba yake.


Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Umeme TANESCO mkoani Kilimanjaro Mhadisi Mahawa Mkaka, alitaka jamii kutoa taarifa kwa shirika hilo pindi wanapotaka kukata au kupangua matawi ya mti ili kufanya tathimini ya athari zinazoweza kujitokeza wakati wa zoezi hilo.

No comments

Powered by Blogger.