Full-Width Version (true/false)


Mourinho apiga ‘stop’ Bale kusajiliwa Man United 
England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameionya bodi klabu hiyo  kuacha mpango wake wa kumwaga fedha ili kumsajili nyota wa Real Madrid, Gareth Bale wakati wa msimu huuu wa kiangazi.
Kauli hiyo ya Mourinho ameitoa ikiwa ni siku chache baada ya kuwapo mpango klabuni hapo kutoka kwa kiongozi wa juu, Ed Woodward kutaka kumnyakua Bale msimu huu.
Mpango wa kocha huyo wa Manchester ni kusajili wachezaji ambao anaweza kudumu nao kwa muda mrefu. Mourinho akili yake anawaza kuwasijili Fred na Sergej Milinkovic-Savic.
Vigogo wa Man United wapo tayari kumjaza noti Bale kiasi cha Pauni 200 milioni.
Licha ya Bale kuisaidia klabu yake kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu lakini anaonekana wazi hana mpango wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Hispania.     

No comments

Powered by Blogger.