Full-Width Version (true/false)


Mpoto abariki ‘uhasama’ wa Diamond, Alikiba

 


Mwanamuziki  Mrisho Mpoto maarufu 'Mjomba', amesema anatamani  ‘uhasama’ uliopo kati ya  Diamond Platnumz na Alikiba uendelee kuwepo daima. 
Akizungumza na MCL Digital, Mpoto amesema uhasamu wao umekuwa wa manufaa katika muziki wa Bongo Fleva na burudani kwa ujumla na kwamba anaona wakipatana  watapoteza ladha ya muziki huo wa Tanzania unaokuja  juu.
"Yaani mwenzenu hilo bifu la Diamond na Kiba nalifurahia sana, limeleta utamu katika muziki, ninachoomba tu libaki katika soko la muziki na lisiwe lile la kushindwa hata kusalimiana.
Mpaka leo naamini wanaowatengenezea uadui ni mashabiki wa muziki wao kitu ambacho ni kizuri kinachowasaidia katika muziki wao" amesema Mpoto aliyejikita katika kughani mashairi.
Mkali huyo wa kibao cha 'Nikipata Nauli' amesema haoni sababu ya wawili hao kutoa nyimbo pamoja kwa kuwa wataharibu utamu mzima wa ushindani wao na kutaka wabaki hivyo hivyo.
Hivi karibuni msanii huyo ameachia kibao cha 'Nimwage Radhi', akimshirikisha  mwanamuziki kutoka WCB, 'Harmonize'.

No comments

Powered by Blogger.