Full-Width Version (true/false)


Msanii Ruby azua kizazaa kingine


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ruby, amesema hawezi kuzungumzia jambo lolote lililomtokea nchini Afrika Kusini alipokwenda kikazi kutumbuiza licha ya watu kudai hakuweza kuimba kutokana na vitu alivyokuwa akivitumia na kumpelekea kupata usingizi mzito na mwishowe kuishia kulala hotelini. 

Ruby ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza mbele ya kamera za eNewz kutoka EATV baada ya mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kufahamu ukweli wa mambo yaliyomsibu kama ni kweli au laa lakini cha kushangaza mwanadada huyo alihamaki na kukimbia 'interview'.

"Kuna sababu nyingi sana za mtu kusafiri na mimi ukiniona nimesafiri basi ujue nimeenda kupiga kazi. Kiufupi watu wa South Africa naweza sema ni 'very peacefully', waelewa wakisema wanapenda kitu basi ujue ni kweli, siwezi kusema ni 'show' ngapi nimefanya nikiwa huko ila huwa naziweka kwenye ukurasa wangu wa instagram", amesema Ruby.

No comments

Powered by Blogger.