Full-Width Version (true/false)


Msukuma: humu Bungeni Wabunge 180 ni Darasa la Saba Wengine Wanafoji Vyeti Kupata Nafasi za U-waziri

Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma Kasheku ameweka wazi anafahamu zaidi wa Wabunge 180 bungeni darasa la 7 ingawa hawapendi kusema ukweli ndiyo maana wanafoji mpaka vyeti ili kupata nafasi za kuteuliwa U-waziri


Akichat Live na wananchi kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kila Jumatano kupitia ukurasa wa Facebook EATV, Musukuma amesema kwamba viongozi wengi wanaojinasibu kuwa wana elimu kubwa ukikaa nao karibu matendo yao hayafanani na viwango vya elimu wanayoisema.

Aidha Msukuma amefafanua kwamba ifike mahali watu wawe wanawajaji wenzao kwa matendo yao na siyo vyeti kwani watu kuamini kwenye vyeti ndiko kunakopelekea watu kwenda kufoji mpaka vyeti.

"Mimi nafahamu mule bungeni kati ya Wabunge 360  Wabunge 180 ni darasa la saba japokuwa hawataki kueleza ukweli. Wametegesha vyeti ili wapate uwzairi. Unamkuta mtu anavyeti ambavyo huko nyuma hakuwa navyo. ukifatilia historia kabla ya kuingia bungeni alikuwa Jobless wengine ma DJ na elimu wanazizisema sijui Cambridge hawana".

Pamoja na hayo Musukuma amesema pamoja na kuwa alisha declare yeye ni darasa la saba ipo siku ataweka wazi kiwango cha elimu yake na kwamba licha ya kuwa ana elimu hiyo yeye ni mtu ambaye anapenda kusoma na ana uelewa wa kupambanua mambo.

No comments

Powered by Blogger.