Full-Width Version (true/false)


Msuva kung'ang'ana na TP Mazembe


Ratiba ya mashindano ya klabu bingwa Afrika inaendelea leo ambapo mchezaji mtanzania Simon Msuva, ataingoza klabu yake Difaa El Jadidi ya nchini Morocco kupambana na timu ngumu ya TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi. 
Mchezo huo wa pili wa kundi B utachezwa leo Mei 15, 2018, katika uwanja wa Stade Al Abdi huko Morocco kuanzia saa 4:00 usiku kwa muda wa Afrika mashariki. 

Timu ya Difaa El Jadidi itahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka matumaini ya kusonga mbele baada ya mchezo wa kwanza kupata sare ya goli 1-1 dhidi ya timu ya MC Alger kutoka nchini Algeria.

Mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha klabu ya ES Setif ambayo haina alama itawakaribisha wageni timu ya MC Alger
Katika msimamo wa kundi B timu ya TP Mazembe inaongoza ikiwa na alama 3 baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa  magoli 4-1 dhidi ya timu ya Es Setif ya nchini Algeria 

Mechi nyingine zitakazopigwa leo ni pamoja na Swallows itakuwa mwenyeji wa timu ya De Agosto, KCCA FC dhidi ya Al Ahly, wakati timu ya ES Tunis wataikaribisha klabu ya Rollers na klabu ya WAC Casablanca itapambana na Togo Port.
 

No comments

Powered by Blogger.