Full-Width Version (true/false)


MTIBWA KUPELEKA MAUMIVU YANGA LEO, KIFARU AELEZA WAKIKAZA SANA WATAKULA NNE

 

Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaikaribisha Yanga katika Uwanja wake wa nyumbani, Jamhuri Stadium leo Jumapili kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wamejiandaa kupeleka maumivu kwa wanajangwani amabao tayari wameshaukosa ubingwa.
Kifaru ameeleza kuwa maandalizi yao yapo vizuri huku akijinadi kwa kutamba kama Yanga wakikaza zaidi basi watafungwa bao nne.
Taarifa zinaeleza kuwa hali za wachezaji na morali kuelekea mtanange huo ziko vizuri na wapo tayari kuzitumikia dakika 90.

No comments

Powered by Blogger.