Full-Width Version (true/false)


Mtibwa Sugar wamepania ubingwa FA


 

Arusha: Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema watatumia nguvu zote kuhakikisha wanakuwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho (FA) watakapovaana na Singida United kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini hapa.

Alisema katika kuhakikisha hilo wamesafiri na kikosi kizima cha wachezaji wake huku kila mchezaji akiwa na hali ya kusaka ubingwa huo kwa namna yoyote.

 “Tangu kuanza kwa mashindano msimu huu hatujacheza katika uwanja wa nyumbani, lakini tumekuwa tukifanikiwa kupata ushindi jambo ambalo linazidi kutupatia ujasili zaidi kwa maana timu zote zitakuwa katika uwanja wa ugenini,” alisema Katwila.

Aliongeza wakazi wa Morogoro pamoja na wapenzi wao wanapaswa kuwaamini licha ya kukabiliwa na mchezo mgumu kwa timu ilijaa wachezaji wengi kutoka mataifa ya mbalimbali na Mtibwa iliyojaa wazawa.

Katika michezo ya Ligi kuu Bara Singida haijafanikiwa kupata matokeo mazuri mbele ya Mtibwa Sugar iliyomaliza nafasi ya sita ikiwa na pointi 38 wakati Singida ikimaliza nafasi ya tano ikiwa na pointi 41.

Hata hivyo Katibu Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Swaburi Abubakar alisema washangiliaji 200 wanatarajia kutua Arusha kwaajili ya kuwapa sapoti kwenye mchezo huo.

 “Hadi sasa mashabiki kutoka Turiani wameshajazi mabasi makubwa matatu na bado Morogoro mjini kuna msafara mwingine ambao wanajikusanya wenyewe hivyo kutakuwa na watu wengi zaidi kuelekea Arusha,” alisema Abubakar.

No comments

Powered by Blogger.