Full-Width Version (true/false)


Mtoto wa miaka mitatu aliwa na chui

Kutoka nchini Uganda, Maafisa wa Wanyamapori wanaendelea kumsaka chui aliyemshambulia na kumla mtoto wa miaka mitatu pamoja na mwangalizi wa Hifadhi ya Taifa ya Queen Elizabeth.

Tukio hilo linaelezwa kutokea Ijumaa ya wiki iliyopita ambapo mtoto huyo anayefahamika kwa jina la Elisha Nabugyere alimfuata mlezi wake nje ya nyumba yao ambayo haikuwa na uzio na ndipo chui huyo alipomuona na kumshambulia.

Msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi nchini Uganda Bashir Hangi ameeleza kuwa mlezi huyo hakujua kuwa mtoto alimfuata nje, lakini alisikia kelele za mtoto huyo kulia na alivyotoka nje chui huyo alitokomea hifadhini na mtoto huyo.

Hangi amesema kwamba siku mbili mbele walipata fuvu la kichwa tu la mtoto huyo.

No comments

Powered by Blogger.