Full-Width Version (true/false)


Muziki sio vita, ukiufanya vita lazima ufeli – Mr. T TouchProducer wa muziki Bongo, Mr. T Touch amesema yeyote anayefanya muziki kama vita ni lazima atafeli.

Kauli ya Mr. T Touch inakuja mara baada ya kumchukua msanii Bgway kutoka Free Nation ya Nay wa Mitego ambapo mwanzoni Mr. T alikuwa akifanya kazi.

“Unajua muziki sio vita, ukifanya muziki vita lazima ufeli, muziki ni kipaji, burudani, unafanya watu wanafurahia maisha, haujawahi kuwa vita ila umewahi kuwa sehemu ya kuwafanya watu waishi maisha mazuri,” amesema.

“Japo huo huo muziki kuna watu wanautumia vibaya kwa kuufanya kama sehemu ya kufanya maovu yao lakini hauko hivyo, ukiutendea mema lazima ukulipe mema,” Mr. T Touch ameiambia Bongo5.

Msanii Bgway baada ya kuanza kufanya kazi na Mr. Touch ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Na Stay.

No comments

Powered by Blogger.