Full-Width Version (true/false)


Mwafrika aliyembadili Buffon kutoka kiungo hadi golikipa bora duniani

Gianluigi Buffon ametangaza kuondoka katika kikosi cha klabu hiyona si kustaafu kama watu wengi ambavyo wanafikiria.

Moja ya mikasa ambayo inamhusu Gianluigi Buffon inawezekana watu wengi wakawa hawaifahamu, Buffon wakati anaanza maisha ya kucheza soka alianza kucheza katika nafasi ya kiungo katika timu ya vijana ya Parma.

Alijiunga na timu hiyo akiwa na umri wa miaka 13 siku moja magolikipa wote wa timu ya vijana wa Parma wote walikuwa wagonjwa, aliyekuwa kocha wa magolikipa Ermes Fulgoni akamwambia Buffon wewe ni mrefu naomba ukae golini.

Buffon akakubali kwa sababu wakati huo alikuwa anamfuatilia mtu mmoja alikuwa akiitwa Thomas N’Kono kwa hiyo wakati anaambiwa hayo maneno na yeye akilini mwake alikuwa ana picha ya Thomas N’Kono kwa sababu alikuwa anamfuatilia sana.

N’Kono alikuwa golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon na yeye alimfuatilia sana katika fainali za kombe la dunia mwaka 1990 ambazo zilifanyika Italia.

Kwa hiyo ushawishi wa  Ermes Fulgoni na yeye mawazo hake pamoja na ushawishi wa aliyekuwa kocha wa magolikipa akabadili nafasi aliyokuwa akicheza kutoka kiungo hadi golikipa.

Kuanzia hapo Buffon akaendelea kuwa golikipa mahiri kutoka Parma kwenda Juventus na leo ameamua kutangaza kuondoka kwenye klabu ya Juventus.

No comments

Powered by Blogger.