Full-Width Version (true/false)


Mwaka mmoja tangu kifo cha Ivan; ‘Najua unatabasamu katika utukufu wa Mungu’ – ZariNi mwaka mmoja sasa umepita tangu aliyekuwa mume wa Zari The Boss, Ivan Ssemwanga ‘Ivan Don’ afariki.
Zari ameeleza jinsi anavyomkumbuka Ivan ambaye walijaliwa kupata watoto watatu pamoja. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;
Mwaka mmoja umepita tangu siku hiyo ya kusikitisha ulipoitwa. Mungu alikuchukua nyumbani kwake, ilikuwa mapenzi yake lakini katika nyoyo zetu bado unaishi.

Najua kwa hakika kwamba hatuwezi kupoteza watu tunaowapenda wanapokufa. Wanaendelea kushiriki katika kila jambo, mawazo na uamuzi tunayochukua.

Upendo wao unaacha kitu katika kumbukumbu zetu.

Mimi na vijana wangu tunapata faraja kwa kujua kwamba maisha yetu yamejitosheleza kwa upendo wako. Wale tunaowapenda hawaondoki wanatembea nasi kila siku. Hawaonekani, hasikikii lakini kila siku wapo karibu nasi, bado tunawapenda na tunawakumbuka.

Najua unatabasamu kutoka katika utukufu wa Mungu. Endelea kupumzika kwa amani Don #CommemoratingIvan #CelebratingIvansLife

Ivan alifariki May 25, 2017, alijipatia umaarufu mkubwa tangu nchini mwake Uganda hadi Afrika Kusini ambako ameacha utajiri mkubwa uliomfanya kuwa mmoja ya watu matajiri nchini humo kabla ya kufikwa na mauti

No comments

Powered by Blogger.