Mwalimu aliyemfundisha Rais Magufuli ajitokeza mbele yake
Mzee aliyejulikana kwa jina la Hermany Raphael Hurry amedai kuwa
aliwahi kumfundisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania somo la
Education Media Technology Mwaka wa tatu katika chuo cha Mkwawa.
Akimtambulisha mbele ya Rais , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Willia Lukuvi alisema watampa nafasi ya kumsalimia Rais kwa
mkono.
“Mh. Rais yuko mzee mmoja Herman Raphael Hurry huyu mzee alifundisha
chuo hiki mwaka 1978 mpaka 1991 kwa kumbukumbu zake anasema alimfundisha
Mh. Rais somo la Education Media Technology Mwaka wa tatu baadae
utapata nafasi ya kumsalimia Mh. Rais kwa mkono,” alisema Lukuvi.
Rais Magufuli leo,alikuwa akizungumza na wanafunzi pamoja na
wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani
Iringa ,
No comments