Full-Width Version (true/false)


Mwanamke auliwa kwa kulazimisha kufunga ndoa



Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Samuel Bariluno katika kijiji cha Nakwaya, wilaya ya Mityana chini Uganda amemuua kwa bastola mchumba wake kwa kile kinachosemekana kuchoshwa na tabia ya mwanamke huyo kukumbushia mara kwa mara suala la kufunga ndoa. 
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo majirani wanasema wawili hao walikua wanatabia ya kugombana mara kwa mara kutokana na marehemu aliyejulikana kwa jina la Agnes Nakimera kutilia msisitizo suala la kufunga ndo na bwana bariluno.

Mashuhuda wanasema kwamba bwana Bariluno ambaye ni mfanyabiashra katika soko la Wakiseka, alimpiga risasi mchumba wake huyo kisha nayeye kutaka kujiua kwa bastola hiyo lakini ilishindikana na badala yake alipata majeraha.

Watoto wa familia hiyo wamesema kwamba wazazi wao walikua wanagalia runinga kabla ya kuanza kujibizana kwa sauti na ndipo walipomuona baba yao akichukua  bastola na kumfyatulia mama yao.

“Baba alichukua bastola na kumfyatulia mama kifuani na baada ya kugundua mama yupo katika hali mbaya akaamua kujiga risasi na kujijeruhi vibaya” alisema mmoja wa watoto wa familia hiyo.

Marehemu Agnes Nakimera alifariki dunia katika kituo cha afya cha Bukomero.

Mkuu wa polisi wa katika wilaya ya Mityana Kamanda John Bosco Serunjoji amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wanamshikilia mtuhumiwa ambaye anatibiwa katika Hospitali ya Rufaa Mulango.
 

No comments

Powered by Blogger.