Full-Width Version (true/false)


Mwanasheria wa Misri amshitaki RamosMwanasheria mmoja kutoka Misri Bassem Wahba, amefungua shitaka kwenye Shirikisho la soka Duniani FIFA, akidai fidia ya  Euro bilioni 1, takribani Trioni 2, kwa mlinzi Sergio Ramos baada ya kumuumiza Mohemed Salah kwenye fainali ya UEFA Mei 26. 

Wahba ametangaza kuchukua hatua hiyo mchana wa leo kwenye runinga ya El Balad TV ya Misri, ambapo ameeleza tayari shitaka lake lipo FIFA, ambapo amedai kuwa yeye anaamini kitendo cha Ramos kilikuwa cha makusudi.

Salah alianguka na kuteguka mfupa mdogo kwenye bega la kushoto baada ya kukumbana na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Wakati anaanguka Salah mkono wake ulionekana kubanwa na Ramos.

"Nimefungua shitaka kuomba fidia, ambayo inaweza kuzidi Euro bilioni 1 (Trioni 2) kwa madhara ya kimwili na na kisaikolojia ambayo Ramos amemsababishia Salah na watu wa Misri kwa ujumla'', amesema Wahba.

Kwasasa jopo la madaktari wa Liverpool na Misri wanashirikiana kuhakikisha nyota huyo anapona na kuitumikia timu yake ya taifa ya Misri kwenye fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Juni 14 nchini Urusi.

No comments

Powered by Blogger.