Full-Width Version (true/false)


Mzee Akilimali atangaza nia kugombea Yanga
Katibu wa baraza la wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali, ametangaza nia ya kuwania uenyekiti ndani ya Yanga huku akisisitiza kuwa anataka kuifanyia Yanga makubwa. 
Mzee Akilimali akizungumza na eatv.tv amesema kuwa mwaka huu amedhamiria kuwania uenyekiti ndani ya klabu hiyo na kikubwa anataka kuifanya Yanga itishe ndani na nje ya nchi.

 "Nina mpango huo na nitagombea kwani lengo langu ni kuifanya Yanga ifanye vizuri ndani na nje ya Tanzania na nimejipanga kukata kiu ya mashabiki wa Yanga" amesema Akilimali.

Mzee huyo aliyeingia mara nyingi katika migogoro na wanachama wa Yanga, aliongea hayo huku akijiamini na kusema kuwa yeye ni mtu sahihi ndani ya klabu hiyo na atagombea muda wakati ukifika

No comments

Powered by Blogger.