Full-Width Version (true/false)


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Masauni amesema Serikali inatambua

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Masauni amesema Serikali inatambua  changamoto zinazolikabili jeshi la polisi nchini na kuwa itakuwa ikitatua changamoto hizo kadri fedha zinavyopatikana. 

Naibu Waziri Masauni amesema hayo Bungeni mkoani Dodoma wakati akijibu maswali ambayo yalielekezwa katika wizara hiyo. 

Amesema moja kati ya changamoto kuu ambayo inalikabili jeshi la polisi ni ukosefu wa magari ya kutosha kwa maaskari polisi hao suala ambalo limekuwa likifanyiwa utatuzi kila fedha zinazopatikana. 

Baadhi ya wabunge walielezea kusikitishwa kwao na hali ilivyo kwa vituo vingi vya polisi nchini na wameitaka Serikali kurekebisha hali hizo.

No comments

Powered by Blogger.