Full-Width Version (true/false)


"Naingiza milioni kwa siku" - ShettaMsanii wa muziki wa kizazi kipya Shetta amesema kwamba licha ya kuwa kimya kwenye game, lakini anaingiza pesa nyingi sana nje ya muziki zinazotokana na biashara ndogo ndogo anazofanya. 

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, amesema kwamba yeye ni miongoni mwa watu ambao wana biashara ya vibanda vya chips vingi, vinavyomuingizia takriban milioni kwa siku.

“Mimi nafanya bishara, nina biashara ndogondogo ambazo nazikusanya pia, ujue mimi ni mmoja kati ya watu ambao wana vibanda vya chips vingi, kwa siku kila kimoja kinatoa laki na nusu au laki mbili, imagine una vibanda vya chips vitano ambavyo kila siku vinakupa laki 2, kwa hiyo nakusanaya milioni kila siku”, amesema Shetta.

Msanii huyo licha ya kufanya biashara hizo, pia anajihusisha na kuwasimamia wasanii wenzake wakiwemo The Mafik Band.

No comments

Powered by Blogger.