Full-Width Version (true/false)


Namshukuru Mungu ametujaalia mtoto wa kike, naumizwa na wanaosema nimegoma – AjibStraika wa klabu ya Yanga, Ibrahim Ajib amejaaliwa kupata mtoto wa kike huku akisema kuwa anashangazwa na watu wanao mshambulia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwamadai kuwa amegoma kusafiri na timu hiyo kwenda nchini Algeria kuwakabili USM Alger mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Namshukuru Mungu ametujaalia kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwa sababu ujauzito wa Mke wangu ulikuwa na matatizo mengi. Kunawakati nilikuwa na hafu kubwa juu ya maisha yake.

Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu yakufanya hivyo, mpira ni kazi yangu.

Nawasamehe kwasababu wangesikia Mke wangu amefariki kwa matatizo ya uzazi nadhani wangesema mengi.
Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga kimesafiri juzi kuelekea nchini Algeria kwaajili ya mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya USM Alger utakao pigwa hapo kesho siku ya Jumapili huku wachezaji wake nyota, Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa, Papy Kabamba Tshimbi na Kelvin Yondani wakikosekana kwenye kikosi hiko kwa sababu mbalimbali.

No comments

Powered by Blogger.