Nape amuaga Kinana kwa ujumbe mzito

Mbunge wa Mtama, na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM, Nape Nnauye amemaga na kumuahidi aliyekuwa Katibu wa chama chao, Ndg Abdulrahman Kinana aliyestaafu leo kuwa wataendelea kumuenzi na mbegu aliyopanda itaota.
Nape
ametoa ahadi hiyo kwa Kinana ikiwa ni muda mfupi baada ya kiongozi huyo
kutangaza kustaafu nafasi hiyo na kukubaliwa na Mwenyekiti wa Chama
hicho na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Pamoja na hayo Nape ameweka wazi kumtambua kinana kama mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma.
"Pumzika rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi
usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili
mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! Umepanda mbegu na
itaota,"
No comments