Full-Width Version (true/false)


''Natamani kukutana na mwenye Instagram'' – FaizaMwanamama asiyeishiwa matukio katika mitandao ya kijamii Faiza Ally, amesema kuwa anatamani kuonana na mwanzilishi wa Mtandao wa ‘Instagram’ kwani amerahisisha maisha yake. 
Faiza amesema kuwa Instagram imemfanya apate pesa pamoja na umaarufu na kupelekea urahisi wa kufanikisha biashara zake.

“Natamani sana nimuone aliyetengeneza Instagram nimwambie ahsante kwa sababu amefanya maisha yangu yamekuwa rahisi sana na amefanya nipate pesa naitegemea sana kulingana na kazi zangu”. Amesema Faiza

Faiza Ally ni mmoja kati ya watu maarufu nchini waliojizolea umaarufu kupitia matukio yake katika mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook na Instagram.
 

No comments

Powered by Blogger.