Full-Width Version (true/false)


Ndoa iliyodumu kwa dakika 15 tu na kuachana

Leo May 30, 2018 stori ninayokusogezea leo ni kuhusu ndoa iliyokuwa imefungwa na wapenzi jijini Dubai imegeuka kituko baada ya wanandoa hao kudumu kwa dakika 15.

Sababu zilizofanya ndoa hiyo kudumu kwa muda mfupi huo imeelezwa kuwa ni makubaliano waliyokuwa nayo kati ya bwana harusi na baba wa bibi harusi ambapo bwana harusi alimkubalia baba wa bibi harusi kutoa mahali ya dola 27,000 sawa na zaidi ya 13,500,000 za kitanzania wakati akitakiwa kutoa nusu ya fedha hiyo kabla ya kufunga ndoa na nusu nyingine baada tu ya kutoka mahakamani kufunga ndoa hiyo.

Inaelezwa kuwa bwana harusi huyo alifanikiwa kutoa nusu ya mahali hiyo kabla ya kufunga ndoa kama alivyoelekezwa na baba mkwe na baada ya kufunga ndoa na kuanza kuondoka kwenye viunga vya mahakama, baba wa bibi harusi alimfata bwana harusi mbele ya ndugu, rafiki na jamaa waliohudhuria ndoa hiyo akitaka kulipwa nusu ya mahali iliyobakia kama walivyokubaliana.

Aidha bwana harusi alimweleza baba wa bibi harusi kuwa fedha zipo ndani ya gari na asubirie kwa dakika 5 tu atampa lakini baba huyo hakuridhika na majibu ya bwana harusi na kumwambia kuwa amtume rafiki yake kwenye gari akazilete fedha hizo na ndipo bwana harusi alipokasirika kwa kuona anadhalilishwa na baba mkwe wake mbele ya watu waliohudhuria ndoa hiyo.

Unaambiwa hivi bwana harusi baada ya kukasirika alirudi ndani ya mahakama na kuvunja ndoa hiyo iliyodumu chini ya dakika 15.
Mwanasheria aliyeshughulikia kesi hiyo amesema kuwa bwana harusi ameona kuwa amefedheheshwa na kudhalilishwa na baba mkwe na ndio sababu iliyomfanya avunje ndoa hiyo na hataki tena mwanamke huyo kuwa mke wake.

No comments

Powered by Blogger.