Full-Width Version (true/false)


Ndoa ya Alikiba Yamkimbiza Jokate Mitandaoni

Miaka kadhaa iliyopita mahusiano ya Alikiba na Jokate yaliingia katika headlines za juu kabisa, hata hivyo baadaye yakuja kuripotiwa kuvunjika lakini hakuna kati yao aliyeweka wazi hilo.

Baada ya Alikiba kufunga ndoa Aprili 19, 2018 na mrembo Aminah kutoka Mombsa Kenya ambaye hakufahamika hapo awali ilithibitisha lilokuwa likizungumzwa lilikuwa na ukweli.

Ndoa Alikiba kila aliyeizungumzia siku hiyo ya April 19, 2018 ilikuwa ni vigumu kuepuka kilitaja jina la Jokate hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.

Siku ya shughuli ya Alikiba Jokate aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram na kuambatanisha na caption iliyosomeka; LoL (Laugh Out Loud). Post hiyo ya Jokate ilienda mbali sana baada ya watu kuhusisha na hatua aliyochukua Alikiba ya kufunga ndoa.

Sasa basi, tangu April 20, 2018 siku moja baada ya Alikiba kufunga ndoa Jokate hajaonekana katika mtandao huo wa Instagram, hivyo hivyo katika mtandao wa Twitter na Facebook, mashabiki wanahoji ukimya wake umesababishwa na nini?.

Hata hivyo utakumbuka March 20, 2018 katika kuadhimisha kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa (Birthday), Jokate aliweka wazi kuwa yupo mbioni kuolewa ingawa hakuweka wazi ni lini na nani atahusika katika ndoa hiyo.

No comments

Powered by Blogger.