Neema yawaangukia Barack Obama na mkewe, wasaini dili nono
Rais
wa zamani wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle Obama wamesaini
dili nono na kampuni ya Netflix inayojihusisha na masuala ya burudani
kwa kurusha vipindi vya TV, Series, filamu na Documentary mitandaoni.
Barack Obama na mkewe Michelle
Obama na mkewe kwenye dili hilo wamesaini kama Mameneja
wazalishaji ambapo kazi yao kubwa itakuwa ni kusimamia na kuhariri
scripts za Filamu, tamthiliya na Documentary kabla ya kuruka. Hii ni kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na NETFLIX
Hata hivyo, Obama naye baada ya kutangazwa kwa dili amesema kuwa
furaha yake ni kuona anaitumikia jamii na kukutana na watu wa kila aina
ili kujionea utofauti.
“One of the simple joys of our time in public service was getting to meet so many fascinating people from all walks of life, and to help them share their experiences with a wider audience. That’s why Michelle and I are so excited to partner with Netflix — we hope to cultivate and curate the talented, inspiring, creative voices who are able to promote greater empathy and understanding between peoples, and help them share their stories with the entire world.”
Licha ya Netflix kutangaza dili hilo mpaka sasa hawajaweka wazi ni
kiasi gani watawalipa wawili hao, kampuni hiyo imekuwa ikiwalipa watu
maarufu mamilioni ya dola kwenye mikataba yake.
Kampuni ya Netflix mwaka 2014 ilitangaza rasmi kuingia barani Afrika
lakini hata hivyo haijapata umaarufu zaidi ukilinganisha na mabara
mengine.
Kwa sasa unaweza kupata habari zetu zote sehemu moja kwa kupitia App
yetu . Pakua sasa kupitia Play Store kwa kubonyeza >>>HAPA
No comments