Full-Width Version (true/false)


Nesi auawa kinyama na kufukiwa pembeni mwa nyumba yake MkurangaMuuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Rosemary Mgombela anadaiwa kuuawa na kisha mwili wake kufukiwa pembeni ya nyumba yake,tukio hilo limetokea leo ijumaa may 25,2018.

Shangazi wa marehemu Veronica Mapunda amesimulia ilivyokuwa huku akimshuku mume wa marehemu huyo kuhusika kutokana na malalamiko aliyokuwa anayapata kutoka kwa marehemu kuwa hawaelewani.

Baada ya kutekeleza unyama huo mwanaume inaelezwa kuwa aliuzika mwili wa Mkewe pembezoni mwa nyumba wanayoishi.

Mamia ya Wananchi wamekusanyika kushuhudia tukio la kuufukua mwili huo.

No comments

Powered by Blogger.