Full-Width Version (true/false)


Neymar aweka wazi 'anacho-miss' Barcelona


 Nyota wa PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr amesema kama mtu akimuuliza anachokumbuka ndani ya Barcelona jibu ni wachezaji wenzake wa Lionel Messi na Luis Suarez ambao walitengeneza ushirikiano mkubwa. 
"Tulikuwa na urafiki mzuri sana kati yangu, Messi na Suarez kwahiyo kitu ambacho siwezi kusahahau ndani ya Barcelona ni kucheza na hao wachezaji wawili ambao daima tulifurahi na tulikuwa marafiki wakubwa," amesema.

Neymar ameyasema hayo kwenye mahojiano na runinga moja ya Ufaransa alipokuwa akiongelea kupona kwake na kurejea rasmi kazini huku ligi ikiwa inaelekea ukingoni lakini yeye amesema yupo imara kwaajili ya fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi.


Neymar amekaa nje ya uwanja tangu mwezi Februari kutokana na kusumbuliwa na kifundo cha mguu wa kulia lakini sasa amepona baada ya kufanyiwa matibabu nyumbani kwao Brazil.

Nyota huyo mwenye miaka 25 aliondoka Barcelona kwenye usajili wa majira ya kiangazi 2018 na kutua PSG kwa dau la rekodi ya dunia Euro 222 zaidi ya shilingi bilioni 500.
 

No comments

Powered by Blogger.