Full-Width Version (true/false)


Ngoma kuelekea Afrika Kusini



Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, anatarajiwa kusafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu. 

Ngoma ambaye alikuwa Yanga alishindwa kuwa sehemu ya kikosi kutokana na majeraha ambayo yalimshika na kusababisha asicheze takribani msimu mzima unaomalizika leo.

Azam FC walifanikiwa kumalizana na kuweza kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wake uliokuwa umesalia.



Akizungumza na eatv.tv Afisa habari wa Azam FC Jaffary Idd amesema kuwa Ngoma amekamilisha usajili wake klabuni hapo na wanatambua kuwa anasumbuliwa na majeraha yaliyopelekea kukaa nje ya dimba kwa muda.


“Donald Ngoma mkataba wake umekwisha na amekuja kwetu na tunafahamu kuwa anatatizo anatakiwa matibabu na tuko tayari na usajili huu utakuwa nguvu kubwa Azam”, amesema Maganga


Mchezaji huyo  anatarajiwa kuelekea Afrika Kusini siku yoyote kuanzia sasa kufanyiwa vipimo vya afya na baadaye matibabu endapo itabainika inahitajika kufanyiwa.
 

No comments

Powered by Blogger.