Full-Width Version (true/false)


NGORONGORO HEROES YAPOTEZA DHIDI YA MALI KUELEKEA AFCON HUKU KABWILI AKIWA BENCHI


Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes kimekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mali katika mchezo wa kuwania tiketi za kushiriki mashindano ya AFCON (U20).

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam, Mali walikuwa wa kwanza kufunga bao mnamo dakika ya 33 kupitia kwa Ousmane Diakite na baadaye katika dakika ya 41, Samadiare Dianka akaongeza la pili.

Bao pekee la kusawazisha kwa Ngorongoro limetiwa kimiani na Paul Peter kwenye dakika ya 42.

Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ngorongoro, Ammy Ninje alimuweka benchi kipa Ramadhani Kabwili na kumpa nafasi Mzanzibari kutoka JKU, Peter Mashauri kucheza nafasi hiyo.


Kutokana na matokeo hayo, Ngorongoro italazimika kushinda mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wa marudiano utakaopigwa mjini Bamako, Mali, Mei 20

No comments

Powered by Blogger.