Full-Width Version (true/false)


Ni kweli wanaume waaminifu Afrika Mashariki wanatoka WCB – HarmonizeMsanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Harmonize amedai kuwa wananaume waaminifu katika mahusiano wanatokea katika label hiyo.
Awali kauli kama hiyo ilitolewa na mmoja kati ya mameneja wa WCB, Babu Tale July 2017.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia Mambo Mseto, Citizen Radio kuwa kitu hicho ni cha kweli kabisa na uaminifu wao umevuka mipaka, sio Bongo tu.

Ni kweli kabisa asilimia mia moja, hamna matukio halafu sisi ndio tunangoza kwa kusalitiwa,” amesema Harmonize.

Alipolizwa kuhusu Diamond kuwahi kuwa na mahusiano na Zari na wakati huo huo kuna taarifa za kurudiana na Hamisa, alijibu kuwa hilo halijui ila kwa upande wake hana mpenzi mwingine zaidi ya Sarah.

No comments

Powered by Blogger.