Full-Width Version (true/false)


NI VITA KUBWA JIJINI MBEYA LEO, MBEYA CITY VS TANZANIA PRISONS
Ukiacha na Mtibwa ambayo itakuwa inaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro le, vita nyingine kubwa kwenye ligi ipo jijini Mbeya ambapo kutakuwa na DABI kati ya Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbeya City wanaingia mchezo wakiwa wameachwa alama 15 na Tanzania Prisons walio na 44 kwenye msimamo wa ligi.

Wakati huo Mbeya City wao wamejikusanyia jumla ya pointi 29 pekee katika michezo 27 waliyocheza msimu huu.

Taarifa kutoka jijini Mbeya zinaeleza wadau na mashabiki wengi wanausubiria kwa hamu mchezo huo wa vuta nikuvute.

Kueleka mechi hiyo, baadhi ya wadau wameipa Prisons nafasi kubwa ya kupata matokeo kutokana na ubora walionao dhidi ya wapinzani msimu huu.

Mechi hiyo itaanza majira ya saa 10 kamili jioni na itarushwa mubashara na kituo cha Azam TV.

No comments

Powered by Blogger.