Full-Width Version (true/false)


Nikistaafu nitamuachia Mwanamke - Mbunge MtoleaMbunge wa Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea amesema kuwa pindi utakapofika wakati wake wa kuachia ngazi jimboni kwake atamuachia mwanamke kiti chake.
Mbunge wa Temeke Mh. Abdallah Mtolea katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Sekondari ya Buza wakifurahia kupokea msaada huo wa taulo za kike.
Mtolea ametoa kauli hiyo mapema leo shule ya Sekondari Buza wakati akipokea msaada ya taulo za kike kutoka EATV kupitia kampeni yake ya Namthamini ambapo amewapongeza kwa kuonesha namna ambavyo wanathamini watoto wa kike na kuahidi kuwa atakapomaliza muda wake atamuachia mwanamke.

“Kwa hiki mnachofanya EATV mnathibitisha kwa vitendo kauli mbiu yenu ya tinga nambari moja la vijana na hii iwe motisha kwenu wanafunzi msome kwa bidii kwani nitakapo staafu nafasi yangu natamani kumuachia mwanamke kiti hiki na nina tamani awe kati yenu nyie wanafunzi wangu”, amesema Mtolea.
Mapema leo timu ya EATV kupitia kampeni ya Namthamini iliwasilisha taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buza Jijini Dar es Salaam.

No comments

Powered by Blogger.