Full-Width Version (true/false)


Nilialikwa kwenye harusi ya Alikiba ila nilikuwa Afrika Kusini – Harmorapa

 

Baada ya ukimya mrefu msanii Harmorapa ameibuka na kueleza sababu ya kilichopelekea kupotea ghafla.
Harmorapa amesema kwa kipindi kirefu alikuwa nje ya Dar es Salaam kwa kuandaa kazi zake mpya ambazo alikuwa akizifanyia nchini Afrika Kusini.

Pia Harmorapa amedai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii waliohalikwa katika harusi ya msanii Alikiba ila alishindwa kuhudhuria kutokana na safari yake hiyo.

“Uongo dhambi, kualikwa nilialikwa sema nilikuwa sipo Dar es Salaam, kwa hiyo ile kuwa mbali ilisababisha kutohudhuria kwenye harusi, nilikuwa bize nasafiri sana,” Harmorapa ameiambia TV E.

Katika hatua nyingine amedai kuwa nia yake ya kumuoa Wema Sepetu ipo pale pale kwani ni kitu ambacho anaamini kipo ndani ya uwezo wake, huku akieleza kama Dogo Janja ameweza kumuoa Irene Uwoya haoni sababu ya yeye kushindwa.

No comments

Powered by Blogger.