Full-Width Version (true/false)


“Nilienda kuvuruga kwa Lowassa”-MusukumaMfanyabiashara na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma amesema kuwa alienda kuvuruga harakati za kuwania Urais kwa aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia UKAWA Edward Lowassa ambaye alihama (CCM) baada ya kushindwa katika kura za maoni. 
Musukuma ameyasema hayo kupitia kipindi cha Kikaangoni ya EATV inayorushwa kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliulizwa kuwa wakati wa kura ya maoni kumtafta mgombea urais CCM alikuwa upande wa Lowassa na alivyohama aliendelea kuwa upande wake?.

Musukuma amejibu kuwa mgombea huyo hakuwa chaguo lake yeye alienda kwa ajili ya kazi maalum na alipokamilisha alipatikana Mgombea wa Urais kutoka Mkoani kwake.

“Unajua zingine ni mbinu tu za kibiashara hata wafanyabiashara wakubwa tunatumia mbinu hizo kwahiyo hata mimi nilienda tu kufanya kazi yangu nilipokamilisha akapatikana mgombea na ambaye ndiyo Rais wa sasa na anatoka kwetu Geita”. Amesema Msukuma.

Mh. Musukuma ameongeza kuwa wabunge wengi wamekuwa hawana ujasiri wa kuzungumza ukweli kitu ambacho yeye anafanya kwa kujiamini.

No comments

Powered by Blogger.