Full-Width Version (true/false)


Nsajigwa,Pondamali kutimuliwa Yanga,Mexime apata shavu

 


IKOSI cha Timu ya Yanga kufanya mabadiliko ya bechi  la ufundi kwa baadhi ya makocha, ambapo Kocha msaidizi wa kikosi hicho Shadrack Nsajigwa pamoja na kocha wa makipa  Juma Pondamali ndio watakao ondolewa na kuongezwa wengine, wakibaki Mwinyi Zahera, Pamoja na Noeli Mwandila katika benchi hilo la ufundi.

Kocha wa Kagera Sugar  Meck Mexime ataongezeka huku nafasi ya Juma Pondamali ikichukuliwa na Razack Siwa ambaye ni raia wa Kenya.  Hii ni kutokana na kikosi hicho kutokufanya vizuri katika msimu huu uliofikia tamati Mei 28 Ligi kuu Vodacom Tanzania Bara.


Msimu huu umemlizika vibaya kwa Yanga ambayo imeshika nafasi ya 3 wakiwa na alama 52 Azam wakiwatangulia mbele kwa pointi 6 na kushika nafasi ya Pili, wakati Mabingwa wapya wa ligi hiyo Simba Sc wakiwa mbele kwa alama 69.

No comments

Powered by Blogger.