Full-Width Version (true/false)


Nyama yafukiwa Sengerema baada ya kugundulika kuwa na kifua kikuu.

 

Idara ya Mifugo katika halmashauri ya wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, imeteketeza zaidi ya kilo 150 za nyama ya ng'ombe mmoja aliyegundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu baada ya kuchinjwa katika machinjio ya wilaya hiyo ili kunusuru afya ya walaji ambao wangeweza kudhurika iwapo wangekula nyama hiyo. 

Hatua ya kuifukia nyama hiyo imefanywa na Mkaguzi wa nyama wilayani humo Dk.Moris Ngiro baada ya ukaguzi kugundua kuwa nyama hiyo ilikuwa na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu ambao ni hatari kwa binadamu.

 Mfanyabiashara wa duka la nyama mjini Sengerema Mapambano Tambalo ambaye ng'ombe wake ndiye aliyegundulika kuwa na ugonjwa huo amewashauri wafanyabiashara wenzake kuwa makini wakati wa kununua mifugo mnadani.

No comments

Powered by Blogger.