Full-Width Version (true/false)


Nyota wa Azam FC aweka rekodi ya pekeeMshambuliaji chipukizi wa Azam FC Shaban Idd Chilunda amejiwekea rekodi ya pekee ndani ya klabu ya Azam FC, baada ya kucheza raundi ya pili pekee kwenye ligi kuu na kufanikiwa kufunga mabao 8. 
Shaban Idd aliumia na kukosa raundi yote ya kwanza kwenye ligi kuu soka Tanzania bara lakini baada ya kufanyiwa matibabu ya goti nchini Afrika Kusini, alipona na kurejea dimbani raundi ya pili ambapo aliwasha moto wa mabao.
Nyota huyo amefanikiwa kufunga Hat-trick yake ya kwanza kwenye ligi kuu na klabu yake ya Azam FC baada ya kufunga mabao hayo matatu jana usiku dhidi ya Tanzania Prison.


East Africa Television imemtafuta msemaji wa Azam FC Jaffar Idd Maganga ili kufafanua rekodi hiyo ambapo Idd ametumia mechi 6 kufunga mabao hayo nane msimu huu huku Azam ikisaliwa na mechi moja dhidi ya Yanga.

Jaffar amesema Idd amefunga katika moja ya mechi ngumu kwenye ligi kuu ikiwemo ya Mtibwa Sugar na Yanga pamoja na Hat-trick kwenye mchezo wa jana ambapo Tanzania Prisons wanashika nafasi ya 4 kwenye ligi.

No comments

Powered by Blogger.