Full-Width Version (true/false)


Okwi ampongeza Juma KasejaMshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi, ametoa pongezi kwa golikipa wa timu ya Kagera Sugar, Juma Kaseja, kwa kufanikiwa kudaka mkwaju wake wa penati ambao ulipelekea timu ya Simba kupoteza mchezo wake wa kwanza katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara. 
Okwi amesema  hayo jana Mei 19. 2018 akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika sherehe za kukabidhiwa kombe la ligi kuu na kuongeza kuwa anajisikia vibaya kutokana na kukosa mkwaju huo wa penati ambao umeharibu rekodi ya timu.

“Kwanza nampongeza kaseja kwasababu amedaka penati lakini vilevile najisikia vibaya kwasababu nimekosa na tumefungwa, kwahiyo kama nilivvosema sisi tunaangalia picha kubwa tumechukua ubingwa na sasahivi tunasherekea na tunatakiwa tufurahie” amesema Okwi.

Okwi ameongeza kuwa anawashukuru wachezaji wenzake wa timu ya Simba kwa ushirikiano aliopata tangu kuanza kwa msimu wa ligi kuu Tanzania Bara na kufanikiwa kuwa kinara wa mabao na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kuwa kitu pamoja  wakati timu ikielekea katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Majimaji mjini Songea.

Jana Mei 19, 2018 katika mchezo wa ligi kuu bara, mkwaju wa penati ya  Okwi ulidakwa na Juma kaseja ambapo ilipelekea timu ya Kagera Sugar kushinda goli 1-0 kupitia kwa mchezaji Edward Christopher aliyefunga kwa kichwa katika dakika ya 85.

No comments

Powered by Blogger.