Full-Width Version (true/false)


Ombaomba wa Kitanzania wakamatwa Kenya


 

Wakazi saba wa Mwanza na Shinyanga wamekamatwa na maofisa usalama katika kaunti ya Nzoia, mjini Kitale wakijihusisha na ombaomba na ulanguzi wa watu kinyume na sheria za Kenya.

Watu hao waliokamatwa jana na maofisa usalama ni Rhonda Makhenzi, Paolo Amos, Mikael Charles, Emmanuel Masudi, Mbekeso Masunga, Mecha Mabundu,na Pendo Njenzi.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Trans Nzoia, Samson Ole Kine amesema watu hao hawakuwa na nyaraka zinazowawezesha kuwa nchini humo na hawakueleza walichokuwa wakikifanya.

Amesema kabla hawajakamatwa, walikuwa wamejificha kwenye nyumba ya wageni na wengine wakiwa wamekodi vyumba katika mtaa wa Laini moja.

Amesema watuhumiwa hao walikuwa wanafanya kazi ya kuombaomba mitaani.
Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa kuwa nchini Kenya kinyume na sheria ya nchi hiyo.

Watu wengine kutoka Tanzania walikamatwa mjini Eldoret wiki mbili zilizopita walipokuwa wakiomba pesa.

“Tuliambiwa watu wengi Eldoret ni matajiri na wakarimu zaidi kuliko watu wa kwetu,” amesema Maria Mapunda, mmoja wa watuhumiwa hao.

Anmesema walipofikishwa mahamani Eldoret walikiri makosa na mahakama ikaagiza warejeshwe Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.