Full-Width Version (true/false)


Picha: Rais wa Malawi, Prof. Arthur Peter Mutharika aungana na wananchi kuuwaga mwili wa kocha, Jack Chamangwana

Rais wa Malawi, Prof. Arthur Peter Mutharika ameungana na wananchi wa taifa hilo kuuwaga mwili wa aliyekuwa mchezaji soka wazamani wa taifa hilo na mwalimu wa mchezo huo, Jack Chamangwana aliyefariki dunia siku ya Jumapili majira ya jioni kwenye Hospitali ya Queen Elizabeth (QECH) nchini humo.

Rais wa Malawi, Prof. Arthur Peter Mutharika (kulia)

Prof. Peter Mutharika ambaye ni rais wa taifa hilo akiwa pamoja na mkewe ‘First Lady Madam’ Prof. Gertrude Mutharika wamejitokeza kwa familia ya mwanasoka huyo mkongwe ambaye pia amepata kuifundisha klabu ya Yanga ya Tanzania na kuipatia ubingwa wa ligi msimu wa mwaka 2005/2006.


 

Rais huyo wa taifa la Malawi ameeleza namna anavyomfahamu, Jack ‘‘Africa’’ Chamangwana kuwa alikuwa mchezaji mwenye ujuzi wa hali ya juu na mtiifu kwenye soka ambapo alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa hilo kilichoshinda ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1978/79.

Picha za matukio mbalimbali nyumbani kwa marehemu, Jack ‘‘Africa’’ Chamangwana nchini Malawi

No comments

Powered by Blogger.