Pinda atoa muongozo kuhusu Tanzania ya Viwanda

Mhe.
Pinda ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa
Kituo cha Taaluma kuhusu nchi ya China kijilikanacho kama Centre for
Chinese Studies yaani CCS, kituo ambacho ni sehemu ya taasisi za Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Mh. Pinda amesema mageuzi ya kiuchumi hususani kupitia ukuaji wa sekta ya viwanda, yanahitaji kuwa na jamii inayopenda kufanya kazi kwa bidii na iliyo tayari kubadilika kifikra.
Uzinduzi wa kituo hicho umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga, ambaye amesema Tanzania ina uhusiano mzuri na nchi ya China lakini inasikitisha kuona kwamba bado kama nchi haijatumia ipasavyo fursa ambazo taifa la China imezitoa kwa Tanzania.
Aidha kituo hicho kilichozinduliwa kimeelezewa kuwa jukumu lake ni kukuza uhusiano kati ya China na Tanzania pamoja na kutumia mafanikio iliyoyapata nchi ya China kwa ajili ya kuharakisha mageuzi ya kiuchumi.

No comments