Full-Width Version (true/false)


Polisi mjini Roma aomba kupiga ‘Selfie’ na Salah

Polisi mmoja jijini Roma ameomba kupiga picha na mshambuliaji hatari wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah wakati walipotua uwanja wa ndege hapo jana siku ya Jumanne kwaajili ya mchezo wao wa ngwe ya pili ya nusu fainali michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Salah alionekana kuwa mwenye furaha na pasinashaka yoyote wakati akishuka Roma ndipo polisi huyo aliyepaswa kuwaongoza wachezaji wa Liverpool akapata nafasi ya kupiga picha ya ‘Selfie’ na nyota huyo anaetikisa vichwa vya mashabiki na wapenzi wa soka duniani.

Liverpool inatarajia kushuka dimbani hii leo majira ya saa 3:45 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kuwakabili AS Roma ugenini huku wakiwa na faida ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 5 -2 kwenye mchezo wa awali uliyofanyika nchini Uingereza.

No comments

Powered by Blogger.