Full-Width Version (true/false)


Promoter maarufu Rwanda ataja sababu za muziki wa nchi hiyo kutofanya vizuriWakati Bongo Fleva imefanikiwa kufika sehemu kubwa japo kwa kidogo, Jay kalambe wa Rwanda ambaye ni mdau mkubwa wa muziki nchini humo amefunguka sababu ya muziki wao kutofanya vizuri.Kalambe ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya Kasuku Entertainment na Application ya Yeyote Music, ameiambia Bongo5 kuwa sekta ya muziki wa Rwanda ni ndogo sana ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama Kenya, Uganda na Tanzania.


“Elimu zaidi zinahitajika kutolewa kwa wasanii wetu na pia ndio sababu nimeamua kuanzisha App ya Yeyote ambayo mtu anaweza kupata muziki wa Rwanda na tayari tumesha wasajili wasanii zaidi ya 200 na tumeanza kuzitangaza kazi zao,” amesema Kalambe. 

Mbali na kufanya shughuli hizo, Kalambe pia ni promoter wa muziki na ameshawahi kufanya kazi na Rayvanny wa WCB.

No comments

Powered by Blogger.