Full-Width Version (true/false)


Raila Odinga,Uhuru Kenyatta wawaomba radhi Wakenya kwa madhara waliyoyapata kutokana na ugomvi wa kisiasaRais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na kiongozi wa muungano wa Nasa, Raila Odinga leo wamewaomba msamaha wananchi kwa madhara makubwa yaliowapata kutokana na ugomvi wao wa kisiasa. 

Viongozi hao wameomba msamaha leo,  wakati wa hafla fupi ya 16 ya maombi ya taifa yaliofanyika jijini Nairobi na kusistiza kuwa kuomba msamaha si dalili ya udhaifu bali ni ujasiri.

Tumefanya kampeni chafu, tumedhalilishana na kuumizana, lakini leo naomba tusameheane na kuanza ukurasa mpya” Kenyatta.

Kenyatta ameweka wazi kuwa ni wakati wa kumuangukia Mungu na kumuomba msamaha ili kuweza kunusuru nchi yao ambayo imejikuta katika machafuko yanayopelekea vifo hasa wakati wa uchaguzi.

Amesisitiza kwamba wamekuwa na mitazamo tofauti ya kisiasa, lakini tofauti zao hazitaruhusiwa tena kuleta maumivu au vifo kwa wananchi.

Kwa upande wake Raila amesema, kwa niaba ya wanachama wa Nasa, anamshukuru Rais Kenyatta kwa kuweza kufikia maamuzi yenye mlengo wa kuwaunganisha na kuondoa chuki.

Tumeamua kuungana na kufanya kazi kwa pamoja, huku tukihakikisha kuwa hakuna raia wa Kenya atakayekufa kutokana na chaguzi za kisiasa,”Raila.

No comments

Powered by Blogger.