Full-Width Version (true/false)


Rais kenyatta awaomba radhi Wakenya bungeni

 Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewaomba msamaha wananchi wake wakati akilihutubia bunge la nchi hiyo ikiwa kuna jambo baya ambalo alilifanya likawaumiza wananchi wake, kwa njia yoyote ile ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwaunganisha kipindi cha uchaguzi. 
Kenyatta ameoomba msamaha huo mapema jana wakati akilihutubia bunge la nchi hiyo ikiwa  ni kawaida kwake kulihutubia bunge mara moja kwa mwaka.

"Forgive me. Nisameheni tuungane, tushirikiane kurekebisha majeraha tusahau yaliyopita," amesema Rais Kenyatta ambapo inaaminika alitumia saa moja na dakika 22 katika hotuba yake.

Akizungumzia kuhusu yeye kukutana na Kiongozi wa Muungano wa Upinzani nchi Kenya , Kenyatta amesema kwamba

Wakati tulipokutana mimi na yeye (Odinga) mapema mwaka jana tulikubaliana kufanya kazi pamoja ili kuijenga nchi yetu hii. Tunaimani kabisa kwamba tutatumia muungano wetu kutatua kero za Wakenya".

No comments

Powered by Blogger.