Full-Width Version (true/false)


Rais Magufuli afunguka kwa nini alikuwa anapenda kufundsha shule za wavulana tu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema wakati anafanya kazi ya ualimu, alikuwa anapenda kufundisha shule za wavulana kuliko za wasichana akihofia usalama wake. 
Akizungumza alipokwenda kutembelea chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa, Rais Magufuli amesema wakati yuko mwalimu bado alikuwa kijana, hivyo aliogopa kuvunja maadili ya ualimu iwapo angeenda kufundisha shule za wasichana.

“Baada ya kumaliza hapa nilienda kufundisha Sengerema High School, lakini field nimefanya Tosamaganga kwa miezi mitatu, Mwanza Sekondari, nimefanya Lugalo, mtaona mnaweza mkaona nilikuwa naenda kufanya field shule za wavulana tu niliogopa shule za wasichana kwa sababu nilikuwa bado kijana, niliona nisije nikaharibu maadili ya ualimu, ambayo nina uhakika na ninyi mmefundishwa vizuri”, amesema rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema hata yeye amesoma katika chuo hiko na alifurahia maisha ya hapo, kwani yamemfunza mengi.

No comments

Powered by Blogger.