Full-Width Version (true/false)


Rais mpya wa Sierra Leone ameapishwa mbele ya wafuasi wake

Rais mpya wa Sierra Leone ameapishwa mbele ya wafuasi wake katika mji mkuu wa Freetown.

Takriban wafuasi 50,000 wa Julius Maada Bio na chama cha SLPP walihudhuria kuapishwa huko.

Viongozi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais wa Sierra Leone ni Rais wa Liberia George Weah, Rais wa Senegal Macky Sall, Rais wa Guinea Alpha Condé,na Rais wa Togo Faure Gnassingbé.

Mtu mmoja ameripotiwa kupoteza maisha katika msongamano wa watu waliokuwa wakijaribu kutizama sherehe za kuapishwa kwa rais Bio.

Vilevile muigizaji kutoka Nigeria Omotola Jalade na mwanamuziki wa Senegal Youssou Ndour walihudhuria sherehe hizo.

No comments

Powered by Blogger.