Full-Width Version (true/false)


Rammy Galis alizwa na michango ya msiba wa Masogange "Michango ya msiba wako imenisikitisha"

Msanii wa filamu nchini Rammy Galis ambaye aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na 'Masogange' amefunguka na kusema taarifa kuhusu michango ya msiba wa Masogange zimemsikitisha na kuahidi kufanya jambo kupitia kazi yao ya pamoja ambayo anategemewa kutoka siku za karibuni.

Rammy Galis amesema hayo kufuatia kuwepo kwa tetesi kuwa michango ya rambirambi ya msiba wa Masogange imepigwa na baadhi ya wasanii ambao walikuwa wakiratibu zoezi hilo

"Sintofahamu ya mchango wa msiba wako zimenisikitisha sana, namuomba Mungu anisaidie ili niweze kutoa kile kitakacho barikiwa katika kazi ya mkono wangu na wako 'Hukumu', Sania yupo kwa niaba yako mpenzi, pumzika salama Agness" aliandika Rammy Galis

Rammy Galis na Masogange walibahatika kufanya kazi pamoja kipindi ambacho walikuwa katika mahusiano na kufanikisha filamu  inayokwenda kwa jina la 'Hukumu' ambayo bado haijatoka, ambapo kwa mujibu wa Rammy Galis mapato ambayo yatapatikana kupitia filamu hiyo amekusudia kufanya jambo kumuenzi Masogange.

No comments

Powered by Blogger.