Rayvanny Ammwagia Sifa Kibao Rosa Ree
Msanii
wa uziki kutoka WCB , Rayvanny amefunguka na kueleze kwa undani
kwanini msanii Rosa Ree ndio msanii pekee wa kike katika remix ya wimbo
wake wa Pochi nene.
Rayvanny
anasema kuwa amekuwa akivutiwa sana na muziki wa Rosa Ree na pia katika
wimbo huu rapper pekee ambaye angeweza ku-fit kutokana na wimbo ulivyo ,
alikuwa ni Rosa Ree na sio mwingine
“Nawakubali
wasichana wote wanaorap lakini Rosa Ree is my favorite wangu naweza
kusema lakini niliona kama atafaa zaidi kutokana na concept ya wimbo
wenyewe,” amesema.
“Ukimsikia anavyo-sound kama Nicki Minaj sio Nicki Minaj, nikaona kwenye biti kama lile ataleta vibe na ndio maana nikaamua kumuweka,” Rayvannuy ameiambia Wasafi TV.
“Ukimsikia anavyo-sound kama Nicki Minaj sio Nicki Minaj, nikaona kwenye biti kama lile ataleta vibe na ndio maana nikaamua kumuweka,” Rayvannuy ameiambia Wasafi TV.
Katika remix ya wimbo huo watakuwepo wasanii Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo Bizness, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.
No comments