Full-Width Version (true/false)


Rayvanny ataja wasanii watakaosikika kwenye Pochi Nene Remix, Bill Nass atoweka

Baada ya wimbo wa Pochi Nene wa Rayvaany ambao amemshirikisha S2kizzy kufanya vizuri kwenye klabu za usiku na mitaani, msanii huyo ameweka wazi orodha yote ya wasanii ambao watasikika kwenye remix ya ngoma hiyo.Remix hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki kutokana na kusikia vionjo kutoka kwenye ngoma hiyo kwa asilimia kubwa imeshakamilika.

Kupitia mtandao wa Instagram Rayvanny amewataja asanii wote ambao watasikika kwenye Pochi Nen Remix ambao ni Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo BiznesS, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.
Hata hivyo mashabiki wamekuwa wakijiuliza maswali mengi kukosekana kwa Bill Nass kwenye orodha hiyo wakati alionekana kwenye kipande cha video sauti yake ikisikika katika ngoma hiyo.

Remix hiyo imetayarishwa na maproducer wawil akiwemo S2kizzy na Rash Don.

No comments

Powered by Blogger.