Full-Width Version (true/false)


Real Madrid walivyosherehekea na kombe la UEFA Hispania, Ronaldo aimbiwa wimbo na mashabiki (picha)Mabingwa wapya barani Ulaya, Real Madrid usiku wa kuamkia leo Mei 28 wamefanya sherehe kubwa ya kuwaonesha mashabiki wao Kombe kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid nchini Hispania.Kabla ya Sherehe hizo jana mchana wabingwa hao walitembeza kombe la UEFA kwenye viunga vya jiji la Madrid wakiwa kwenye gari maalumu la wazi.Kilichosisimua zaidi wakati wa sherehe hizo ni pale mshambuliaji wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo aliposimama na kutoa hotuba fupi ambayo hata kabla ya kumaliza hotuba hiyo wachezaji wenzake na mashabiki walimkatiza kwa kuimba wimbo uliokuwa unasikika kwa maneno ya “Ronaldo Stay, Ronaldo Stay”. Tazama video na picha za matukio yote.
No comments

Powered by Blogger.